Na Theonestina Juma, Missenyi
WANAFUNZI wa wenye mahitaji maalumu wa Shule ya Msingi Bunazi Wilayani Missenyi, wameiomba serikali kutafuta namna ya kuwapatia chakula kwa kuwa fedha wanazopatiwa na wafadhili kwa ajili hiyo hazitoshi.
Wanafunzi walitoa ombi hilo kupitia kwa Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho, Bw. Wilson Samuel.
Wanafunzi hao wenye ulemavu walisema hawana chakula cha uhakika kwani kilichopo hakitoshelezi licha ya kuwepo wafadhili wanaotoa lishe.
Walisema fedha zinazotumwa kwa ajili ya chakula hakikidhi mahitaji ,hivyo serikali inapaswa kuingilia kati kuwasaidia.
Pia wanafunzi hao walisema kituo hicho akina hata bweni moja hali inayowafanya wazazi kutumia muda mwingi kuwapeleka shuleni watoto asubuhi na jioni kuwafuata ili kuwarudisha nyumbani.
Bw. Samule alisema hiyo ya Bunazi iliyoazishwa mwaka 1956 ikiwa ni shule ya kati kwa sasa inayo jumla ya wanafunzi 1,071 na walemavu 35 kati yao wasichana 12 na wavulana 23.
Alisema shule hiyo ina kitengo cha wanafunzi walemavu wa akili 12, wavulana wanane na wasichana wanne, ambapo kitengo hicho kinahudumiwa na walimu wawili na wengine watatu wako masomoni.
No comments:
Post a Comment