tangazo

Friday, May 27, 2011

Kasi ya utoaji mikopo yapungua

Na Livinus Feruzi, Bukoba

KASI ya utoaji wa mikopo katika Chama cha Akiba na Mikopo Bukoba SACCOS imepungua tofauti na ilivyokuwa mwanzoni kutokana na baadhi ya wanachama kushindwa kurejesha fedha wanazokopo.


Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Bukoba SACCOS, Bw. Goodluck Malemo alipozungumza na waandishi habari.

Bw. Malemo alisema mwaka 2008 jumla ya wanachama 753 walipatiwa mikopo yenye thamani zaidi ya milioni 358.3, wakiwemo wanachama binafsi na 400 na vikundi 353.

Alisema mwaka 2009 mikopo yenye thamani ya milioni 258.2.

Alifafanua kuwa mwaka 2010 idadi ya waliopatiwa mikopo ilipungua hadi kufikia wanachama 168.

No comments:

Post a Comment