tangazo

Thursday, May 26, 2011

Polisi yamshikilia dereva halmashauri Shinyanga

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia dereva wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Abdalah Mkoma (36) Mkazi wa Kitongoji cha Ushirika mjini humo kwa tuhuma za kumgonga mwendesha pikipiki na kusababisha vifo vya watu wawili.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Diwani Athumani alisema dereva huyo aliyekuwa akiendesha gari mali ya halmashauri hiyo alimgonga mwendesha pikipiki Bw. Maganga Gideon (30) Mkazi wa Ngokolo.

Kamanda Athumani alisema, ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:10 usiku katika Barabara ya
Swymarton eneo la Sekondari ya Buluba mjini Shinyanga.

Alisema, mwendesha pikipiki huyo alikuwa amebeba abiria wawili katika pikipiki yake ambapo yeye pamoja na abiria mmoja Bi. Mary John (31)
Mkazi wa Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga walikufa papo hapo.

Alisema, abiria mwingine aliyekuwa amebebwa katika pikipiki hiyo aliyetajwa kwa jina la Bi. Matlida Njega (22) Mkazi wa Lubaga Manispaa ya Shinyanga alijeruhiwa vibaya.

Alisema, mtu huyo alivunjika mguu wake wa kulia na hivi sasa amelazwa katika hospitali ya serikali mjini Shinyanga akipatiwa matibabu na hali yake inaelezwa kuwa nzuru.

Kamanda Athumani alisema, mara baada ya ajali hiyo dereva wa gari hilo alitoroka na kwenda kusikojulikana ambapo hata hivyo juzi saa 5.20 asubuhi ambapo sasa yupo chini ya ulinzi wa polisi.

No comments:

Post a Comment