Na Livinus Feruzi, Bukoba
TATIZO la vijana kutopenda kushiriki shughuli za
kilimo na ufugaji na badala yake kukimbilia kuendesha baiskeli na pikipiki ni changamoto kubwa inayoikabili Manispaa ya Bukoba.
Hayo yalisemwa na Kaimu Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika Manispaa ya Bukoba Bw. Josephat Kyebyara,wakati akikabidhi vyeti kwa wahitimu 24 wa kikundi cha shamba darasa.
Alisema vijana wengi wanataka kupata fedha za haraka ndiyo maana hawapendi kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali.
Bw. Kyebyara alisema hata wazazi wengi wamekuwa wakielekeza vijana kufanya kazi ya kuendesha pikipiki badala ya shughuli zingine.
Alisema sio lazima mtu kukaa shambani muda wote tangu asubuhi hadi jioni akilima.
“Ni kweli tunaweza kukubali kwamba kilimo kinawachelewesha kuwapatia fedha, lakini mtu akiamua kulima au kufuga kisasa anaweza kubabili maisha yake," alisema.
Kutokana na hali hiyo aliwashauri vijana kujenga tabia ya kupenda kushiriki shughuli
za kilimo na ufugaji ili waweze kujiongezea kipato.
Wakizungumza na majira kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi katika manispaa ya
Bukoba walisema vijana wengi hawapendi kufanya kazi za kutumia nguvu
No comments:
Post a Comment