tangazo

Friday, May 27, 2011

Chuo cha ualimu chajengwa Kyerwa

Na Theonestina Juma, Kyerwa

CHUO kipya cha ualimu kimeanzishwa katika wilaya mpya ya Kyerwa, mkoani Kagera ambapo hadi kukamilika kwake kinatarajia kugharimu sh. bilioni 2. Chuo hicho kinatarajiwa kufunguliwa Julai, mwaka huu.


Kwa mujibu wa mmiliki wa chuo hicho ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, Bw. Eustance Katagira mradi wa ujenzi wa chuo hicho ulianza Juni, mwaka 2009 katika Kijiji cha Katera, Kata Isingiro Tarafa ya Kaisho/ Murongo wilayani humo.

Bw. Katagira alisema chuo hicho kinatarajiwa kufunguliwa Julai mwaka huu kikiwa na wanachuo 720 wa jinsia zote na hadi sasa mradi wa ujenzi huo umeshagharimu sh. milioni 500 kati ya sh. bilioni 2 zinazokisiwa kutumika baada ya kukamilika kwa majengo yote ya awamu ya kwanza.

Alisema sababu za kujengwa kwa chuo hicho katika wilaya hiyo mpya ni baada kutokana na kukabiliwa na upungufu wa walimu.

Alisema kutokana na hali hiyo, aliona kuunga mkono jitihada za seriklai za kupambana na kuondoa upungufu wa walimu kwa kujenga chuo cha ualimu kikiwa ni mojawapo ya kitengo katika kituo kikubwa cha elimu (Kyerwa Education Centre).

Alisema mradi wa huo umenza na awamu ya kwanza ukiwa na jengo la utawala, majengo manne yenye vyumba 12 vya madarasa na maabara.

Pia ujenzi wa mabweni, jiko, bwalo na vyoo vya nje tayari usanifu wa michoro na ununuzi wa vifaa vya ujenzi umeishakamilika ambapo maandalizi hayo yanaenda sambamba na ujenzi wa matanki ya kuvuna maji ya mvua na usanifu wa nyumba za walimu.

Alisema chuo hicho kitatoa mafunzo ya ualimu daraja la tatu ‘A’, stashahada na wanafunzi kurudia masomo. Alisema chuo hicho kina mpango wa kufundisha shahada.

Pia uongozi wa chuo una mpango wa kujenga chuo cha Kilimo, mifugo na uvuvi na kujenga sekondari ya kidato cha tano na sita.

5 comments:

  1. Litakuwa ni jambo la muhimu sana kwani mkoa wa Kagera umerudi nyuma sana kielimu jambo ambalo pamoja na mambo mengine limechangia sana kuporomoka kwa uchumi wa wananchi wa mkoa huo.

    ReplyDelete
  2. safi sana! waheshimiwa na wengine wote wenye uwezo mkoani kagera wangeiga mfano huu wa mbunge wa Kyerwa.

    ReplyDelete
  3. Mh ni vema kuwa na moyo kama wa mh mbunge huyu pasipo kujari ni akina nani watasoma kwenye hiyo chuo kwa manufaa ya kusaidia nchi yetu, tunaitaji hata akina Mbowe wanaomiliki makasino dar zinazochangia vijana kupoteza maadili na huku wamiliki wakijionyesha kuwa wanaitakia mema serikali kumbe ni danganya toto, toa mfano wa kupunguza matatizo yanayoikabiri serikali na wa wala sio kuharibu vijana kwa kumbi za sitarehe.

    ReplyDelete
  4. Nchi yetu ina rasilimali nyingi ziwezazo kutatua matatizo yote hapa nchini.Uongozi wa kuzisimamia ndo hamna,kinachohitajika ni kuwezesha maendeleo ya Taifa na sio ujenzi wa chuo kwa hela za kuomba omba!

    Huu mie naona ni mradi tu,kwani ni mali ya mbunge tuache kudanganyana!Pia si kweli kuwa Karagwe ni maskini wa kuomba omba eti wajengewe chuo!

    Wee unaona mbunge ndo mmiliki harafu unasifu eti maendeleo ya watu wote.Huoni ni sawa na mtu kubuni mradi wowote baada ya kuona biashara hiyo inalipa eneo hilo!

    La muhimu hapa,hili la chuo cha mbunge lisihusishwe katika mada za eti ni msaada wake kwa wananchi!Asimamie hekali za ardhi ya viongozi wa serikali hii waliojigawia bure huko kagera sugar irejeshwe,wananchi wapate pa kuchungia mifugo yao!

    Ndg,mbunge tetea watu,acha sifa zinazochefua wasomi wa Karagwe,simamia rasilimali zao ili wafaidi nchi yao!!

    ReplyDelete
  5. Asante sana mbunge kwani hatua hiyo inaonesha uzalendo wako kwa Wanakyerwa,tunatarajia kuona mambo mazuri zaidi.

    ReplyDelete