tangazo

Thursday, May 26, 2011

Michango iliyochangwa Kagera Day na jinsi ilivyotumika

*Ni harambee iliyoongozwa na Lowassa
*Sh. milioni 196 bado zipo kwa watu

WAKAZI wengi wa Kagera wamekuwa na shauku ya kujua ni jinsi gani michango iliyotolewa wakati wa uzinduzi wa Siku ya Kagera zilivyotumika. Kamati ya Kagera Day kwa kuzindua ziku hiyo iliendesha harambee. Katika makala haya, Mwandishi Wetu, anaeleza mchanganuo wa ahadi zilipatikana jinsi zilivyotumika. Hii ni kulingana na mchanganuo uliotolewa na Kamati ya Kagera Day.


CHIMBUKO la Kagera Day ambayo sasa inaitwa Kagera Yetu, ni haja ya wana-Kagera waishio nje ya mkoa wa Kagera kutaka kushiriki na kushirikishwa katika maendeleo ya mkoa wa Kagera. Ni imani ya waasisi wa dhana hii kuwa wakiweza kujenga utamaduni wa kila mwananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ya taifa kama vile ilivyo kwenye shughuli za kijamii za harusi, kipaimara na kuzikana bila kuitegemea serikali pekee, kasi ya kujenga taifa itaongezeka kwa kiwango cha kuridhisha.

Kagera Day:

NOVEMBA 27 2007 iliyokuwa siku ya uzinduzi wa siku ya Kagera. Kamati ya Kagera Day kwa kuizindua siku hiyo iliendesha harambee kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam kwa kuwakutanisha watu zaidi ya 500.

Mgeni Rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete, lakini kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine, aliwakilishwa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa.

Jambo la historia katika siku hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera wakati huo, Bw. Enos Mfuru kuongoza a timu ya viongozi wa mkoa na wale wa wilaya nane za mkoa wa Kagera ili kuhamasisha Watanzania kushiriki kuijenga Kagera.

Matakwa ya wakati huo ilikuwa ni kuwaunga mkono wananchi wa mkoa wa Kagera katika ujenzi wa shule za sekondari za kata na kauli mbiu ilikuwa ni JENGA KAGERA TUIENDELEZE TANZANIA.

Makusanyo

Wakati wa harambee hiyo ilipokelewa a ahadi zinazogawanywa katika mafungu makuu matatu. Moja, kulikuwa na ahadi za fedha na pesa taslimu. Katika fungu hili zilipatikana kiasi cha karibu sh millioni 480 na hii ni kutoka kwa washiriki waliohudhuria siku hiyo.

Zilikusanywa sh. Millioni 280 ambazo ni sawa na asilimia 58.3 ya ahadi zote katika fungu hili. Hadi sasa kiasi ambacho hakijakusanywa ni sh. million 196 sawa na asilimia 41.7 ya ahadi zote katika fungu hili.

Fungu la pili ni michango iliyotolewa na halmashauri zote za wilaya za mkoa wa Kagera. Zote zilitoa ahadi ya sh.i millioni 20 kila moja ambazo jumla yake ni sh. million 160 katika kundi hili. Kutokana na pilikapilika za kukamilisha madarasa ya sekondari mwanzoni mwa mwaka 2008 iliamuliwa fedha hizo zielekezwe kwenye miradi moja kwa moja badala ya kuwekwa kwenye akaunti ya pamoja.

Hamasa ya Kagera Day ilikuwa chachu tu, kazi iliyofanyika ni kubwa zaidi ya kiasi hicho. Kwa kazi hiyo halmashauri zote zimepongezwa

Kundi la tatu lilikuwa ni la ahadi ya vifaa mbalimbali vya ujenzi, vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano, ahadi za kukamilisha miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na ahadi ya ujenzi wa shule ya mfano (model school).

 Ahadi zote katika kipengele hiki zilithamanishwa kuwa sh. million 840. Tathimini ya wanakamati wa Kagera Day hadi sasa ni utekelezaji wa ahadi katika fungu hili, utaweza kufikia kiwango cha asilimia 85.7 bila kuwa na uhakika wa ahadi za vifaa na miradi inayokadiriwa kufikia sh. millioni 120 kama itatekelezwa ambayo
ni sawa na asilimia 14.3

Ahadi zote katika mafungu hayo matatu zina thamani karibu sh. billion 1.5 na makusanyo yanawaweka katika asilimia 77.3 ya utekelezaji, kiwango ambacho kwa kuanzia kinatia moyo. Kwa watu wanaotumia lugha ya darasani hiyo ni B+ au upper second. Kamati inashukuru walioshiriki na wanaounga mkono jitihada hizi, inawezekana.

Ufafanuzi wa ahadi za vitu halisi (si fedha)

Tanzania Eduaction Authority (TEA), wamejenga madarasa mawili Shule ya Sekondari Nono iliyopo Karagwe na madarasa matatu Shule ya Sekondari Ijuganyondo ya Bukoba mjini. Vodacom Tanzania, wamejenga madarasa matatu Shule ya Sekondari Bugene ya Karagwe, Bw. Ansel Katanga wa London Uingereza alitoa kompyuta 51 ambazo zilisambazwa kwenye sekondari nane moja kutoka kila wilaya.

Shule ya mfano iliyotolewa na Professa Anna Tibaijuka, inajengwa katika kata ya Mayondwe, wilaya ya Muleba mpakani mwa wilaya ya Muleba na Bukoba kilomita tano toka Bandari ya Kemondo. Kamati inashukuru wananchi wa Mayondwe kwa kutoa ardhi bila malipo kwa ajili ya mradi huo.

Vingamuzi toka Multchoice, Madishi manane kutoka multichoice yamefungwa katika sekondari zenye umeme ili kusaidia kutoa elimu kwa kuona. Simbanet na mtambo wa internet, mtambo huu umefungwa katika halmashauri ya Biharamulo.

Mgawanyo wa rasilimali zilizokusanywa

Kamati inaeleza kwa muhtasari kanuni ya uendeshaji wa shughuli za Kagera Day. Kamati ya Kagera Day ni timu ya uhamasishaji, ni kikosi cha kupanga mbinu na mikakati ya kuwaunganisha wadau ili washiriki kujiletea maendeleo.

Rasilimali zinazopatikana kama ni fedha uwekwa benki kwenye akaunti maalum kama ni vifaa mdau uelekezwa avipeleke Bukoba au mkoani sehemu itakayoamuliwa na uongozi.

Kamati uwasiliana na ofisi ya mkoa kwa rasilimali zilizopo na kuomba mkoa uratibu wapi rasilimali hizo zielekezwe. Viongozi wa mkoa ambao ni RC, RAS na REO (kwa shughuli za elimu) uwasiliana na uongozi wa wilaya hasa wakurugenzi. Mdau anayekuwa amependekezwa na Mkurugezi na kupitishwa na uongozi wa mkoa kamati ya Kagera Day anatumiwa hundi kupitia mkoani. Kamati haina mamlaka ya shule gani inufaike iko wazi kiasi hicho.

Iliamuliwa zijenge maabara sita za mfano kutokana na ukweli kuwa ni asilimia nane tu za sekondari mkoani Kagera zilikuwa na maabara mwaka 2007. Sasa kiwango hiki kitakuwa kimepungua sana kutokana na ongezeko la sekondari za kata. Nia ni kuwa angalau na maabara moja kila tarafa.

Majina ya sekondari hizo na wilaya zilizo kwenye mabano ni kama ifuatavo; Rubondo (Biharamulo) , Kagondo (Muleba), Izimbya (Bukoba Vijijini), Makyurugusi (Chato), Bunazi (Missenyi) na     (vi) Shyunga (Ngara).

Majengo tajwa hapo juu yote yameezekwa yakiwa katika hatua za ukamilishaji (finishing) na kutokana na uhitaji wa vyumba vya madarasa baadhi ya shule zinayatumia kama madarasa. Zikipatikana kiasi cha ya shillingi millioni 90 majengo yote yatakamilika kabisa.

Ujenzi wa vyumba vya madarasa

Vodacom (T) waliahidi na kutujengea madarasa matatu katika sekondari ya Bugene Karagwe, TEA walituahidi na kutujengea madarasa mawili sekondari ya Nono Karagwe na madarasa matatu Ijuganyondo iliyoko Manispaa ya Bukoba. Ni kutokana na mgawo wa vyumba vya madarasa ambavyo wachangiaji (wahisani) walikuwa na uhuru wa kuchagua wapi wajenge halmashauri hizi mbili hazikujengewa maabara.

Angalizo: Ujenzi wa madarasa na maabara tajwa hapo juu haukushirikisha
nguvu za wananchi. Mifuko ya saruji 150 yenye thamani ya sh. millioni 3 iliyoahidiwa na NBC Ltd iligawanywa kwenye halmashauri nane kama ilivyoainshwa hapa chini:

Bukoba (M) mifuko 15, Bukoba (V) mifuko 20, Biharamulo mifuko 20, Karagwe mifuko 15, Missenyi mifuko 20     , Muleba mifuko 20, Ngara mifuko 20 na Chato mifuko 20. Mgawo wa saruji mifuko 800 ya Celtel sasa Zain nao ulifuata utaratibu wa hapo juu kwa kila wilaya kupata mifukpo 100.

Mgawo wa mabati 600 yaliyotolewa na MM Intergrated Steel Mills Ltd kila wilaya ilipatiwa mabati 75.

Mgawo wa Kompyuta 51 zilizotolewa na Computer for Africa ltd ya London chini ya uongozi wa Bwana Aseri Katanga ulifanyika katika sekondari na idadi zake kwenye mabano.

Biharamulo - Biharamulo SS (6), wilaya ya Chato sekondari ya Nyamirembe ( 6) Bukoba (V) sekondari ya Maruku (6) , Missenyi sekondari ya Bunazi ( 6) Bukoba (M) sekondari ya Rugambwa (6), Muleba sekondari ya Kishoju (7) Ngara sekondari ya Ngara (7) na Karagwe sekondari ya Bugene ( 7).

Mgawo wa fedha za maabara zilitumwa kwa shule husika baada ya kuteuliwa na wilaya na kupitishwa ofisi ya mkoa na kila jengo limegharimu kama ifuatavyo:

Sekondari ya Kagondo sh. milioni 38, Bunazi sh. milioni 40.454 , Shyunga sh. milioni 38,    (iv) Izimbya sh. milioni 38, Makyurugusi sh.milioni 38 na Rubondo sh. milioni 38.l


No comments:

Post a Comment