tangazo

Friday, May 27, 2011

DC asema siasa imeingia Burigi

Na Theonestina Juma, Biharamulo

MKUU wa Wilaya ya Biharamulo, Bw. Ernest Kahindi amesema uharibifu wa pori la Nyantakara na Burigi umefikia asilimia 40 kutokana na kuingiwa na masuala ya kisiasa.


Mkuu huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa kikao cha ushauri wa mkoa.

Alisema na masuala ya kisiasa kutawala wilaya hiyo, kumesababisha kuingilia hifadhi ya mazingira, ambapo uharibifu huo umefikia asilimia 40 katika pori la akiba la serikali la Nyantakara na Burigi.

Alisema maeneo hayo licha ya kufanyiwa msako (operation) ya mara kwa mara ni kama robo tu.

Alisema kutokana na uharibifu kuzidi kukithiri katika maeneo hayo, bila nguvu ya serikali ya mkoa kuingialia vitendo hivyo vitaendelea.

Bw. Kahindi alisema katika hifadi hizo, watu kutoka maeneo mbalimbali wamekuwa wakivamia hifadhi hiyo na kuchoma mkaa, kupasua mbao na vitendo vingine viovu.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Bw. Alponary Mugalula, tatizo kubwa katika eneo hilo pia ni mifugo wilaya ya Magu.

Mkuu wa Mkoa Kagera, Bw. Mohamed Babu, alisema msako wa watu wanaoharibu mazingira hayo unatakiwa uwe wa kudumu na si kazi ya mara moja tu.

Kuhusu mifugo kutoka wilaya moja hadi nyingine, alisema inatakiwa mtu kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine kufuata utaratibu wa kutoa taarifa kuanzia ngazi ya kijiji kama kupata kibali.

No comments:

Post a Comment