tangazo

Thursday, May 26, 2011

MUWAWATA yatetea wanajeshi wastaafu

Na Livinus Feruzi, Bukoba

MUUNGANO wa wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA) Mkoa wa Kagera umesema nchi nyingi duniani zimeingia kwenye matatizo baada ya
wanajeshi wastaafu kukaa bila kazi na hatimaye kuchoshwa na hali ya maisha tofauti na walivyozoea awali.


Wanajeshi hao walibainisha hayo mwishoni mwa wiki kwenye risala yao iliyosomwa kwa niaba yao na Kaimu Mwenyekiti MUWAWATA, Bw. Richard Kashombo, wakati wa mkutano wao wa kutambulisha muungano huo
mkoani wa Kagera.

Walisema wanajeshi wanapostaafu na kuanza kuishi uraiani bila kazi baadhi yao wanachoshwa na hali hiyo.

Bw. Kashombo alisema cha kusikitisha kuona serikali inaendelea kuwatunza kwa kuwapatia kiasi kidogo cha fedha ikilinganishwa na veo alivyokuwa navyo.

Walisema licha ya kwamba kiasi hicho hakikidhi mahitaji kulingana
na maisha ya sasa

Alisema pamoja na kustaafu kazi bado wana nguvu za kulitumikia taifa kama walivyokuwa wanafanya wakati wakiwa kazini.

Wanajeshi hao wastaafu walimuomba mkuu wa mkoa wa Kagera kuwapatia shughuli zote za usafi, na kutunza mazingira kwa kadiri ya sheria za
mkoa wa zinavyoelekeza.

Pia waliomba kupewa kazi mbalimbali kulingana na taaluma zao zikiwemo ujenzi wa madarasa ya shule, madaraja, barabara, na utengenezaji wa
samani za shule na kuomba serikali kuwatumia pale yatakapo tokea maafa yoyote mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment