HALI YA UTENDAJI KAZI
Watendaji wapo wanne, miongononi mwao mmoja ni mkuu wa idara na mwingine ni mratibu wa TASAF. SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA IDARA
UTOAJI WA MIKOPO
Jumla ya vikundi 12 vya wanawake na kimoja cha vijana vimepata mkopo kwa
kipindi cha mwaka 2009 hadi 2011.
CHANGAMOTO
Baadhi ya vikundi havirejeshi mkopo kwa wakati hivyo kusababisha udumavu wa mfuko wa wanawake na vijana.
HUDUMA NA MISAADA
Kulipa karo na mahitaji muhimu kwa wanafunzi yatima walioko Sekondari na vyuo mbalimbali. Kwa kipindi cha mwaka 2010 zaidi ya sh. 11,000,000/= zimetumika katika shuguli hii. Vikundi vingine 19 vilipata mkopo usiyo na riba kupitia mfuko wa microkrediti tangu mwaka 2009 hadi 2010.
Wanawake 50 waishio na VVU/UKIMWI wamepewa msaada wa lishe.
CHANGAMOTO
Idadi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wanaohitaji msaada wa masomo ni kubwa sana ukilinganisha na fedha ambazo kwa kiasi kikubwa zinazotolewa na wahisani kwa ajili ya kuwalipia gharama za masomo hivyo kutofikia malengo yaliyopangwa.
Baadhi ya vikundi vilivyokopa kupita mfuko wa microcredit mwaka 2009 havijarejesha na hivyo kufanya kiasi cha deni kuwa shilingi 2,545,272.45/=
KUTOA ELIMU
Mafunzo ya ujasiliamali
Vikundi mbalimbali vya ujasiliamali vimekuwa vikipata elimu hususani kabla ya kuanzisha vikundi. Jumla ya Wanawake 55 waishio na UVV/UKIMWI wamepewa mafunzo ya ujasiliamali na kuhamasisha waanzishe vikundi kwa ajili ya kupatiwa mikopo, mafunzo haya yalitolewa mwaka 2010.
CHANGAMOTO
Baadhi ya vikundi vinahitaji zaidi ruzuku kuliko mikopo kwa sababu ya kutokujiamini katika shughuli zao hivyo wanahofia hasara ambayo inaweza kusababisha kushindwa kurejesha kwa wakati.
Elimu ya UKIMWI
Elimu ya UKIMWI imekuwa ikitolewa katika jamii kwa mfano kipindi cha mwaka 2010 elimu hii imetolewa kwa Watumishi 40 wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba namna ya kujikinga na VVU, kuepuka maambukizi mapya na maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
CHANGAMOTO
Unyanyapaa bado ni tatizo katika utekelezaji wa shughuli za UKIMWI kwa sababu waathirika wengi bado hawajajiweka wazi na hili linaweza kuchochea maambukizi mapya.
No comments:
Post a Comment