tangazo

Thursday, March 17, 2011

SEKTA YA USAFIRISHAJI

1. UTANGULIZI
Sekta ya usafirishaji ni sekta inayohusika na masuala yote yanayohusu usafiri na usafirishaji katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba.

2. KAZI ZINAZOFANYIKA KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI.
1. Kusimamia na Kuratibu masuala  yote yanayohusu usafiri na usafirishaji.

2. Kusimamia Madereva na kuhakikisha wanatekeleza kazi zao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.
3.  Kusimamia na Kuratibu matumizi ya magari, mitambo, pikipiki na mafuta.
4.  kuandaa taarifa na kuziwasilisha sehemu husika.
5. Kuchambua na kukadiria takwimu za usafirishaji.
6. Kukadiria na kushauri juu ya utendaji wa kazi mbalimbali za sekta ya usafirishaji.
7. Kushiriki katika kupanga mikakati ya kuendeleza mtandao wa Usafirishaji.
8. Kukusanya takwimu mbalimbali kwa ajili ya kutayarisha bajeti ya sekta ya usafirishaji.

3. CHANGAMOTO.
1. Magari kuwa katika idara hali inayopelekea usimamizi na
     uratibu kuwa mgumu hali hii usababisha kuwepo
     muingiliano wa kimaamuzi.
2. Ukosefu wa mfumo wa Computerized TMIS (Transport Management Information System).
3. Kutokuwepo na ratiba za kazi za kila mwezi katika Idara.
4. Kutokuwepo kwa akaunti maalum kwa ajili ya sekta ya Usafirishaji.
5. Upungufu wa Madereva
6. Upungufu wa ujuzi kwa baadhi ya Madereva.
7. Upungufu wa vitendea kazi.
8. Ufinyu wa bajeti inayotengwa katika kulipia bima, kununua mafuta na kutengeneza magari.
4. MAPENDEKEZO / MAONI.
1. Kuwepo kwa kitengo maalum cha matumizi ya magari
(‘Transport Pool’).Au baadhi ya magari yawe kwenye pool ili
Kurahisisha utendeji kazi kwa idara ambazo hazina magari.
2. Idara zitoe ratiba za kazi kila mwanzo wa mwezi husika.
3. Halimashauri iangalie uwezekano wa kufungua akaunti maalum ya usafirishaji.( ‘retention account’ )
4. Halmashauri iajili Madereva wa kutosha ikilinganishwa na idadi ya magari.
5. Madereva wachache waliopo wapelekwe katika chuo cha Taifa cha Usafirishaji ili waongezewe ujuzi katika fani ya udereva.
6. Halmashauri inuunue vitendea kazi vya kutosha ili kufanikisha shughuli zote za usafirishaji.
7. Halimashauri ya Manispaa itenge fedha za kutosha kwa ajili ya matengenezo na kulipia bima.
Pamoja na hayo nashauri upungufu na mapendekezo/Maoni tajwa hapo juu yafanyiwe kazi.
Naomba kuwasilisha.

Lucy Emily Bakuza.
Afisa Usafirishaji wa Manispaa,
BUKOBA.

No comments:

Post a Comment