tangazo

Thursday, March 17, 2011

KUSHUKA KWA ELIMU KATIKA MKOA WA KAGERA

01: UTANGULIZI: Mkoa wa Kagera upo Magharibi mwa nchi yetu ya Tanzania. Unazo wilaya saba ambazo b Bukoba, Biharamulo, Chato, Karagwe, Missenyi, Muleba na Ngara. Makabila yaliyopo katika mkoa huu ni Wahaya, wanyambo, wahangaza, Wasubi na wasukuma. Mazao ya chakula ni ndizi, mihogo, viazi vitamu, viazi vikuu, maharage na njugu mawe. Mazao ya biashara ni pamoja na
kahawa, pamba na ndizi. Mkoa wa Kagera hupata mvua katika msimu wa vuli na masika.
HALI YA ELIMU
Mkoa wa Kagera ulikuwa na hali nzuri sana ya kielimu kuanzia miaka ya 1960 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1980. Wananchi walikuwa na mwamko mkubwa sana wa elimu na vijana wengi walijiunga na shule za msingi wachache waliendelea na elimu ya sekondari katika shule za serikali na wachache  walikwenda kusoma katika shule za sekondari nchini Uganda. Elimu mkani Kagera ilipewa kipaumbele cha kwanza kwani wanafunzi waliokuwa na tatizo la upatikani wa mahitaji ya shule walipata msaada toka mfuko wa chama cha Ushirika na BCU(Buoba Cooperative Union) na hatimaye KCU 1990 LTDkupitia  mfuko wa Elimu (Balimi Education  Fund) Kutokana na jitihada za chama cha Ushirika cha Wakulima wa Kahawa (Buni) Kagera wanafunzi wengi waliendelea na masomo  yao hadi chuo kikuu. Wazazi na wananchi kwa ujumla walihakikisha watoto wote wenye uwezo wa kusoma wanasoma. Vijana waliohitimu Darasa la Nane, Kidato cha Nne na kuendelea masomo wengi walifanikiwa kupata ajira hivyo kuboresha maisha yao na familia zao. Mwanzoni mwa mwaka 1980 Elimu mkoani Kagera ilianza kuorora kutokana na sababu zifuatazo:-
1. VITA YA KAGERA:
Nchi yetu iliingia vitani na nchi ya Uganda maarufu kwa VITA YA KAGERA. Vita hivi vilisababisha watu wengi kupoteza maisha pamoja na mali zao. Ucchumi wa  mkoa na nchi yetu kwa ujumla ulidorora sana na maisha ya wananchi yalibadilika.
Vita ilidumu kwa muda mfupi lakini madhara yake yanaonekana hadi leo. Baada ya vita wanafunzi na watumishi wengi waliacha shule na kazi na kuingia kenye biashara na walitengeneza fedha nyingi kwa muda mfupi. Vijana wengi waliona nibora kufanyabiashara badala ya kuendelea na masomo shuleni. Wafanyakazi nao waliona ni bora kufanyabiasha kulikokuendelea na kazi za serikali ambazo zilikuwa hazilipi vizuri, kana kwamba hiyo haitoshi, ugonjwa wa UKIMWI ukaingia katika nchi yetu  ukitokea Uganda. Watu wengi walipoteza maisha bila kujua ni ugonjwa gani ulikuwa ukiwasumbua. Wanafamilia walitumia muda mwingi kuhudumia wagonjwa badala ya kufanya kazi  za uzalishaji mali ama wanafunzi kwenda shule. Pigo hilo linaendelea hadi leo. Pesa nyingi zilitumika kuboresha afya badala ya kulipia karo za wanafunzi.
Aidha  watoto wengi wanalazimika kujilea na kulea wadogo zao badala ya kuhudhuria shule.
2. KUSHUKA KWA BEI YA BUNI (KAHAWA)
Suala linalosababisha kudorora kwa elimu mkoani hapa ni kushuka vibaya kwa bei ya kahawa katika soko la dunia. Hali hii iliathiri sana uwezo wa wana Kagera kumudu gharama za masomo kwa watoto wao ndani na nje ya nchi. Aidha hali hii ilisababisha kuporomoka kwa chama cha KCU 1990 LTD pamoja na mfuko wa Elimu wa chama hicho uliojulikana kama “Balimi Education Fund”
3. UKOSEFU WA KAZI AU AJIRA:
Katikati ya miaka ya 1990 Serikali ilishindwa kuajiri watumishi wapya na mwishoni mwa miaka  hiyo ililazimika kupunguza watumishi wake (retrenchment) Watumishi waliopunguzwa katika sehemu zao za kazi walilipwa kiinua mgongo lakini fedha hizo ziliisha ndani ya muda mfupi na maisha yao yakawa katika hali mbaya. Vijana wengi walihangaika  huko na kule kutafuta ajira bila mafanikio na elimu yao ikaonekana haina maana yoyote.
4. MATARAJIO YA WAZAZI:
Wazazi walipokuwa wanatumia rasilimali zao kuwasomesha watoto wao walitazamia wapate kazi na wawasaidie kuwatunza wazazi wao pamoja na ndugu zao au familia zao. Baada ya wahitimu kukosa kazi wazazi walikata tamaa na kuvunjika moyo na hawakuona umuhimu wa kutumika rasilimali zao kuwasomesha watoto wakati hakuna ajira.
5. UGONJWA WA ZAO  LA MIGOMBA
Ugonjwa wa migomba maarufu kama “Myauko” umeongeza umasikini mkoani Kagera kwa sababu ni zao la chakula linalopendwa na watu wengi. Wananchi wananunua ndizi kwa bei kubwa na hivyo kukosa pesa za kuwalipia watoto wao gharama za kielimu.
      6. MWAMKO WA KIELIMU KATIKA MIKOA MINGINE
Tangu  enzi za uhueu wa nchi yetu mikoa iliyokuwa inaongoza kielimu ni Kilimanjaro, Mbeya na Kagera. Kwa sasa mikoa ambayo ilikuwa imejikita kwenye ufugaji na biashara za kuni na mkaa imeanza kukimbizana na elimu. Mkoa wetu upo pembezoni mwa nchi na hamna fursa kama mikoa ya wenzetu. Hali hii imeufanya mkoa wetu urudi nyuma zaidi kielimu maana ushindani umekua mkubwa zaidi.
7. JANGA LA MELI YA MV. BUKOBA
Kuzama kwa Meli ya Mv. Bukoba lilikuwa pigo kubwa kwa mkoa wetu maana walimu wengi waliopangwa Kagera waligoma kuja kwa kisingizio  ch kuogopa kuzama katika ziwa kwa vile njia ya uhakika wa kuja mkoani Kagera ilikuwa kupitia ziwa Viktoria mbaya zaidi hata vijana waliozaliwa Kagera baadhi yao waligoma kuja kufanya kazi hapo. Hali hii imesaidia sana kuishusha Kagera kielimu.
8. MATUMAINI MAPYA WANAKAGERA
Baada ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutuunganisha na mikoa jirani hali ya kielimu imeanza kuboreka Kagera. Mnamo miaka ya 1990 mkoa  Kagera ulikuwa unashika nafasi ya kumi na tisa kitaifa, lakini kwa sasa mkoa wa Kagera ni kati ya mikoa minne bora kielimu nchini.
9. JUKUMU LA MWANAKAGERA
Ni jukumu letu wana Kagera kuendeleza mkoa wetu kielimu. Elimu ni muhimu sana kwa watu wetu hata kama hakuna ajira ya kutosha. Hivyo kila mmoja kwa nafasi yake ajione kuwa anadeni la kuinua kiwango cha elimu. Ipo haja ya kuitisha mikutao ya hadhara ya kuhamasisha wananchi wafufue ari ya kuhakikisha watoto na wao wenyewe wanatoa kipaumbele cha kwanza kwa elimu. Walimu  wathaminiwe na wapewe ushirikiano wa kutosha kuitenda kazi yao.
Kamati za shule na WDC ziwashawishi wananchi  na wazazi kuchangia na kuindeleza elimu. Irudishwe mifumo ya wanakagera ya kuwasisia wazazi wa wanafunzi wenye kipato kidogo kwa mikopo yenye masharti nafuu , wale wote wanaopenda kijiendeleza kielimu. Watafutwe  wafadhili wa ndani na nje ya mkoa wa Kagera wawekeze katika Elimu hapa kwa gharama nafuu hasa kwa kujenga Vyuo Vikuu. Wanakagera waishio nje ya mkoa huu wawajibike kufufua umaarifa wa mkoa wao maana mkataa kwao hanatofauti na mtumwa.
Imeandaliwa na:

Idara ya Elimu ya Msingi
Manispaa ya Bukoba
21/01/2011

No comments:

Post a Comment