Kumb. Na. BMC/M.10/6/ 26/1/2011
Mkurugenzi wa Manispaa
S. L. P. 284
BUKOBA
IDARA YA AFYA
Idara ya Afya, katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba inashughuli na utoaji wa huduma za tiba na kinga katika vituo 16 za kutolea huduma za Afya.
AINA YA KITUO | MMILIKI | |||||
Serikali | Mashirika ya Dini | Mashirika ya Umma | Binafsi | Jumla | ||
1 | Hospitali | 1 | 0 | 0 | 0 | 1 |
2 | Vituo vya Afya | 2 | 0 | 0 | 1 | 3 |
3 | Zahanati | 8 | 1 | 1 | 2 | 12 |
Shughuli zinazofanyika
2. Udhibiti wa magonjwa ya Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu na Ukoma
3. Utoaji wa huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto.
4. Utoaji wa huduma ya ukusanyaji na uzoaji wa taka ngumu (Udhibiti wa taka)
5. Udhibiti wa magonjwa ya mlipuko na kukabiliana na majanga
6. Ukaguzi wa majengo mbali mbali ya kuishi, biashara na taasisi na kuhimiza usafi
7. Usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni za afya
8. Utoaji wa elimu ya afya kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara, vikundi vya sanaa na vyombo vya habari.
9. Ukaguzi wa maeneo ya wazi, makaburi, vyanzo vya maji, mifereji, viwanja vya michezo na maeneo ya mikusanyiko.
Mafanikio
1. Kupungua kwa kiwango cha wagonjwa wa malaria kwa asilimia 2% kutoka 40.2% mwaka 2008 hadi 38.2% mwaka 2010.
2. Kuongezeka kwa kiwango cha uchanjaji kutoka 89.1% mwaka 2009 hadi 90%.
3. Kiwango cha maambukizi ya UKIMWI yamepungua kutoka 10.6% hadi 8.4% mwaka 2010 na jamii imehamasika kupata huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya UKIMWI
4. Kuongezeka kwa vyombo vya kusomba taka ngumu kutoka magari/trekta 2 hadi 8 kwa msaada wa UN HABITAT (trekta 4 kubwa na 2 ndogo)
5. Kujengwa kwa maghala (vizimba) 4 ya kuhihifadhia taka katika maeneo ya soko na yenye msongamano wa watu
6. Halamashauri ilipokea magari 2 ya kubeba wagonjwa (Ambulance) na kupeleka Kituo cha Afya Rwamishenye na Zahanati ya Kashai
Changamoto
1. Upungufu wa madawa muhimu kulingana na mahitaji ya vituo
2. Ukosefu wa matanuru ya kuchoma taka zilizosibika (taka za hospitali)
3. Ufinyu wa bajeti ya kwa ajili ya utoaji wa huduma za afya ikiwemo usafi
4. Utiririshaji ovyo wa maji taka mitaani na kwenye mifereji ya maji ya mvua na hatimaye kwenye vyanzo vya maji.
5. Kujaa kwa eneo la makaburi ya Kishenge na kutokuwepo kwa eneo mbadala kwa ajili ya maziko
6. Ukosefu wa maeneo ya kukusanyia taka katika maeneo mbali mbali ya Kata hasa kata za mjini kati
7. Sekta binafsi na asasi za kijamii kutofanya kufanya shughuli za usafi katika eneo la Manispaa kama wakala.
8. Upungufu wa watumishi wa kada mbali mbali
9. Ujenzi holela wa makazi katika maeneo oevu, kando kando ya vyanzo vya maji (mto Kanoni) na kwenye maeneo yenye mawe.
10. Uchakavu wa miundo mbinu hasa mifereji ya maji ya mvua katika maeneo ya barabara za Manispaa
11. Kutobomolewa kwa baadhi ya vichochoro katika maeneo kadhaa za Manispaa
12. Kuzagaa kwa wafanya biashara ndogo ndogo (wamachinga) katika mitaa mbali mbali eneo la mjini kati ambao ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira ya mji.
13. Wananchi kutozingatia sheria na kanuni za kiafya.
14. Ukosefu wa miundo mbinu thabiti (pavement) katika barabara zote za lami na kusababisha mchanga kujaa barabarani hatimaye kujaa na kuziba mitaro.
15. Upungufu wa vyoo vya umma katika maeneo mengi yenye shughuli za kijamii na biashara
16. Ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, mifereji, maji nk katika maeneo yenye msongamano (squatters)
Mikakati/Mwelekeo:-
1. Kuomba madawa kutoka Bohari Kuu ya madawa (MSD) kulingana na mahitaji ya vituo vyetu na kuweka bajeti ya nyongeza mwaka 2011/2012
2. Kuendelea kuhamasisha jamii kuwa na tabia ya kujitokeza kupima afya zao kwa hiari na kupata ushauri nasaha
3. Kuweka bajeti kwa ajili ya ujenzi wa matanuru ya kuchomea taka za hospitali
4. Kuhimiza Halmashauri kutenga eneo jipya la makaburi na kuliwekea uzio tayari kwa matumizi sanjari na kufunga eneo liliojaa la makaburi ya Kishenge
5. Kuhimiza Kamati za Maendeleo za Kata na Mitaa kutenga maeneo ya kukusanyia taka kabla ya kupelekwa dampo
6. Kuomba kibali cha kuajiri watumishi wa kada mbali mbali hasa madereva kwa magari ya taka.
7. Kuhamasisha asasi za kijamii na binafsi kufanya shughuli za usafi wa Manispaa.
8. Kudhibiti ujenzi holela katika maeneo ya vyanzo vya maji hasa mto Kanoni na maeneo oevu kwa kushirikisha Idara ya Mipango Miji na Uhandisi
9. Kukarabati mifereji mibovu ya maji ya mvua katika maeneo mbalimbali ya barabara za Manispaa kulingana na bajeti
10. Kupitia mikakati iliyopo ya usafi wa mazingira kwa kutambua ufanisi/upungufu na kuboresha kulingana na rasilimali zilizopo.
11. Kuwafikisha mahakamani watu wote ambao wanakiuka sheria na kanuni za afya katika mahakama ya papo kwa papo.
12. Kuendelea kuhamasisha jamii kubadili mtazamo na tabia ya kuzingatia usafi na kuchukia uchafu kusudi kuboresha afya na usafi wa mazingira
13. Kuendelea na mikakati ya ukaguzi wa majengo ya kuishi, taasisi na biashara na kuhimiza usafi.
14. Kuhamasisha na kuhimiza wananchi kushiriki kuweka safi maeneo yao kila wiki, siku ya alhamisi ambayo ni Siku ya Usafi katika Manispaa.
15. Usafi wa Manispaa kuwa miongoni mwa vipaumbele katika mipango ya Halmashauri kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2011/2012.
16. Kushirikisha sekta binafsi na asasi za kijamii kujenga vyoo vya umma katika maeneo mbali mbali yenye mikusanyiko ya watu.
Dr. Raphael Kiula
MGANGA MKUU WA MANISPAA
BUKOBA
No comments:
Post a Comment