IDARA YA UTUMISHI NA UTAWALA
UTANGULIZI
Idara ya utumishi na utawala ni idara inayohusika moja kwa moja na usimamizi wa rasiliamli watu na kuhakikisha idara nyingine zinapangiwa watumishi kulingana na Ikama ya idara husika.
Halmashauri ya Manispaa Bukoba ina jumla ya watumishi wapatao 1,205 kati ya hao watumishi 1148 wameajiriwa katika masharti ya kudumu na watumishi 57 ni watumishi wa muda (vibarua)
Idara ya utumishi ni idara mtambuka ambayo inahusika kupanga na kuandaa bajeti ya mishahara ya watumishi na kuhakikisha watumishi wanapata haki zao.
SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA IDARA
Baadhi ya majukumu yanayotekelezwa na idara hii ni pamoja na
i) Kupandisha watumishi vyeo kwa kushirikiana na bodi ya ajira na TSD Wilaya kwa upande wa walimu.
ii) Kuthibitisha watumishi kazini kwa kushirikiana na bodi ya ajira.
iii) Kusimamia zoezi zima la ujazaji wa fomu za OPRAS yaani upimaji wa kazi kwa watumishi
iv) Kusimamia sheria, kanuni, zinazohusu watumishi
v) Kushughulikia malipo kwa watumishi wanaostaafu kazi, mirathi na stahili nyingine.
vi) Kuandaa mpango wa mafunzo kwa kupitia (TAA) Training Need Assesment
Pamoja na kazi nyingine hizo ni baadhi ya kazi zinazofanywa na Idara hii.
CHANGAMOTO
i) Bajeti finyu ya mafunzo inayopelekea kutopatikana fursa ya kutosha kwa watumishi kwenda kwenye mafunzo
ii) Upungufu wa watumishi hususan Idara ya Elimu, Afya na kilimo.
iii) Ukosefu wa vitendea kazi hususan kwa watendaji wa Kata na Mitaa.
iv) Ukosefu na uelewa wa kanuni na sheria zinazohusu watumishi kwa watumishi wenyewe.
Magedi Magezi,
Kaimu: Afisa Utumishi na Utawala
MANISPAA BUKOBA.
No comments:
Post a Comment